Friday, August 12, 2011

BAADA YA KIPIGO BRAZIL YAFUTA MECHI ZAKE MBILI ZA KIRAFIKI.


BRASILIA, Brazil
SHIRIKISHO la Soka Brazil (CBF) limetangaza mechi mbili za kimataifa za kirafiki baina ya timu hiyo na timu za Italia na Hispania kuwa zimefutwa.

Vigogo hao wa soka wa Amerika Kusini walipanga kucheza na mabingwa hao wa mwisho wa Kombe la Dunia kati ya October na November, lakini mechi zote hizo zimefutwa bila maelezo yoyote.

Badala yake Brazil itacheza na Misri jijini Cairo September 6, Costa Rica Oktoba 7 na Mexico siku nne baada ya mechi ya Costa Rica.

Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni muda wa saa 24 tu baada ya kufungwa na Ujerumani mabao 3-2 ambapo Kocha wa Brazil alielezea kipigo hicho kama maandalizi mazuri.

Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia pia watakutana na Argentina mara mbili ambapo katika mchezo wa kwanza ambao utachezwa Argentina itakuwa ni Septemba 14 na kurudiana September 28.

No comments:

Post a Comment