Tuesday, February 18, 2014

NITAFANYA KILA NALOWEZA KUHAKIKISHA NAISAIDIA LIVERPOOL - CISSOKHO.

BEKI wa kushoto wa klabu ya Liverpool, Aly Cissokho anatambua kuwa sio aina ya mchezaji ambaye ni maarufu lakini ameapa kucheza kwa bidii wakati akiwa Anfield. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Liverpool toka uanze mwaka huu lakini amekuwa akishambuliwa na baadhi wachambuzi wa mambo ya soka akiwamo Michael Owen kwa jinsi anavyomiliki mpira na anavyoshambulia. Na wakati akikiri kuwa hawezi kumridhisha kila mtu, amepania kuonyesha thamani yake mpaka mwishoni mwa msimu wakai uamuzi utakapotolewa kama anaweza kupata mkataba wa kudumu kutoka Valencia. Cissokho amesema malengo yake ni kujituma kadri anavyoweza kwa ajili ya Liverpool na kufurahia kila dakika halafu itajulikana huko mbele itakavyokuwa. Beki huyo alicheza mechi yake ya kwanza kwa toka chukuliwe kwa mkopo kutoka Valencia Agosti 24 katika mchezo wa ligi dhidi ya Aston Villa lakini siku tatu baadae alipata majeruhi yaliyomfanya akae nje ya uwanja kwa wiki sita.

No comments:

Post a Comment