Monday, March 9, 2015

BEKI WA ZAMANI WA LIVERPOOL AMPONDA BALOTELLI KUWA MZIGO KWA TIMU.

BEKI wa zamani wa klabu ya Liverpool, Mark Lawrenson amemshambulia Mario Balotelli baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia kushindwa kubadili matokeo katika mchezo dhidi ya Blackburn Rovers jana. Balotelli alitokea benchi katika kipindi cha pili cha mchezo huo war obo fainali ya Kombe la FA uliochezwa katika Uwanja wa Anfield lakini alishindwa kubadili matokeo kwani timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Nyota huyo sasa anakuwa amecheza mechi tano za mashindano bila kufunga bao huku akiwa amefunga mabao manne pekee toka atue Liverpool akitokea AC Milan kwa kitita cha euro milioni 20. Aklihojiwa Lawrenson alimponda Balotelli na kudai kuwa hana msaada wakati anapohitajika na anadhani hakustahili kuwa na timu hiyo.

No comments:

Post a Comment