MSHAMBULIAJI nyota Diego Costa amebainisha kuwa alikaribia kujiunga na Liverpool mwaka mmoja kabla ya kusajiliwa na Chelsea. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mzaliwa wa Brazil alisajiliwa na Chelsea kwa kitita cha euro milioni 40 akitokea klabu ya Atletico Madrid katika kipindi cha majira ya kiangazi ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao 17 katika mechi 21 za Ligi Kuu alizocheza. Costa alifungiwa mapema msimu huu baada ya kumkanyaga mchezaji wa Liverpool Emre Can katika mchezo baina ya timu hizo hivyo kumfanya kukosa mechi za timu yake dhidi ya Manchester City, Aston Villa na Everton. Nyota huyo amesema alikaribia kuondoka Atletico lakini baada ya kupambana na kuanza kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo aliona haina maana kuondoka. Costa aliendelea kudai kuwa aliamua kubakia Atletico kipindi badala ya kwenda Liverpool ili aweze kuimarika zaidi.
No comments:
Post a Comment