OKWI APELEKA KILIO KINGINE JANGWANI WAKATI SIMBA WAKIENDELEA KUITAMBIA YANGA.
KLABU ya soka ya Simba imefanikiwa kuendeleza kwa wataji wake jadi Yanga baada ya kuibuka kidedea katika mchezo baina yao uliochezwa katika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bao pekee lililofungwa na Mganda Emmanuel Okwi katika dakika ya 52 lilitosha kuipa Simba ushindi huo muhimu wa bao 1-0 uliowafanya kuweka hai matumaini yao katika kinyang’anyiro cha Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika mchezo huo kiungo mahiri wa Yanga Haruna Niyonzima alijikuta akipewa kadi mbili za njano na kujikuta akitolewa katika dakika ya 74 na kuifanya timu yake kucheza wakiwa pungufu kwa dakika takribani 16. Pamoja na Kipigo hicho Yanga bado wanaendelea ushikilia usukani wa ligi wakiwa na alama 31 wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 30 na timu imekwea mpaka nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 26.
No comments:
Post a Comment