Sunday, March 8, 2015

POGBA AAMUA KUBAKIA JUVENTUS.

WAKALA wa kiungo Paul Pogba amedai kuwa mteja wake amekubali kubakia Juventus kwa kipindi kirefu na yuko tayari kukataa ofa kutoka katika klabu za Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich na Chelsea. Pogba mwenye umri wa miaka 21 amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu na kufanya kuhusishwa na tetesi za kuwahama mabingwa hao wa Serie A katika majira ya kiangazi. Nyota huyo ana mkataba mrefu na Juventus ambao utamalizika mwaka 2019 na wakala wake Mino Raiola amesema Pogba anataka kumaliza mkataba wake. Raiola amesema amezungumza na rais wa klabu Andrea Agnelli, wakurugenzi Pavel Nedved, Beppe Marotta na Fabio Paratici ambapo wote wakubali kuwa klabu haihitaji fedha kwasasa hivyo Pogba ataendelea kubakia.

No comments:

Post a Comment