MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amesema kikosi chake hakiko katika mbio za ubingwa wa La Liga na kudai kuwa wako katika mapambano binafsi na Valencia na Sevilla kugombea nafasi ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Atletico wangeweza kupunguza pengo la alama mpaka kufikia tano dhidi ya vinara wapya wa La Liga Barcelona lakini walishindwa kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Valencia wanaoshika nafasi ya nne na kujikuta wakipata sare ya bao 1-1. Matokeo hayo yanamaanisha Atletico wako juu ya Valencia kwa tofauti ya alama moja huku Sevilla nao wakiwa katika nafasi ya tano wakitofautiana kwa alama tano. Akihojiwa Simeone amesema mapmbano yao sasa hivi sio kwa ajili ya kutetea taji lao walinyakuwa msimu uliopita kwani bado wanapambana na Valencia na Sevilla ili kuhakikisha wanafuzu michuano ya Ulaya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment