Friday, December 4, 2015

PEREZ ADAI MADRID HAIPASWI KULAUMIWA KUMCHEZESHA MCHEZAJI ASIYESTAHILI.

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema Shirikisho la Soka la Hispania-RFEF ndio linapaswa kulaumiwa kwa klabu hiyo kumtumia mchezaji asiyeruhusiwa katika michuano ya Kombe la Mfalme. Winga Denis Cherychev mwenye umri wa miaka 24 alifunga bao katika mchezo wa juzi walioshinda mabao 3-1 dhidi ya Cadiz, lakini taarifa zilidai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Urusi hakupaswa kucheza kwakuwa alikuwa na adhabu ya kutocheza mechi moja. Perez amesema hajaambiwa chochote kuhusiana na suala hilo hivyo anadhani lawama zinapaswa kuwaendea RFEF weneywe. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kama hawakufahamu lolote hadhani kama wanapaswa kupewa adhabu yeyote. Cheryshev ambaye alikuwa kwa mkopo Villarreal msimu uliopita alikuwa na adhabu kiporo ya mechi moja ambayo aliipata baada ya kupata kadi za njano tatu mfululizo katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment