Wednesday, October 12, 2011

LIVERPOOL WALILIA HAKI ZA MATANGAZO YA TELEVISHENI.

Mkurugenzi Mtendaji Liverpool fc, Ian Ayre.

MKURUGENZI Mtendaji wa klabu Liverpool Ian Ayre amesema kuwa kila klabu kubwa za Uingereza zinatakiwa ziruhusiwe kuuza haki za matangazo ya televisheni zenyewe.

Ligi Kuu ya Uingereza ambayo ndio ligi tajiri kuliko zote duniani kwasasa wanauza haki za matangazo ya televisheni kwa pamoja ambazo zina thamani inayofikia dola bilioni 5 (shs. trilioni 8) katika kipindi cha 2010 hadi 2013 ambapo mgao unakuwa sawa kwa klabu zote 20 zinazoshiriki ligi hiyo.

Hatahivyo Ayre amesema kuwa Liverpool wako tayari kuleta changamoto mpya kuhusu makubaliano hayo wakidai kwamba klabu kubwa zinatakiwa kupewa mgao mkubwa kutokana na kuwa na mashabiki wengi zaidi katika sehemu zingine kama katika bara la Asia.

Ayre anaamini klabu kama Liverpool, Chelsea, Manchester United na Arsenal zinatakiwa kuuza haki za matangazo yake kila moja kivyake kama zinavyofanya timu za Real Madrid na Barcelona za Hispania.

USHAHIDI WA VIDEO KUWASILISHWA KESI YA BIN HAMMAM.

Jack Warner (kushoto) akiwa na Mohamed Bin Hammam

SAKATA la aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Mohamed Bin Hammam limechukua sura mpya baada ushahidi wa video unaomwonyesha aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Jack Warner akiwashawishi wajumbe wa Shirikisho la Soka la Caribbean (CFU) kupokea zawadi kutoka kwa mgombea huyo.

Maelezo ya Warner yaliyorekodiwa aliyokuwa akiwapa wajumbe wa CFU Mei 11 mwaka huu ndio yatakayotumika kama ushahidi katika Kamati ya Maadili ya FIFA kusikiliza mashtaka dhidi ya wajumbe hao wiki hii.

Picha ya video ambayo imechapishwa katika mtandao wa Telegraph unaonyesha Warner akiwaambia wajumbe wa CFU hawalazimishwi kumpigia kura Bin Hammam katika uchaguzi wa urais wa FIFA lakini amemwambia aje na fedha.

Bin Hammam alifungiwa maisha kujishirikisha na shughuli zozote zinahusiana na mchezo wa soka Julai mwaka huu na Kamati ya Maadili ya FIFA lakini amekata rufaa.

Hotuba hiyo ya Warner aliitoa alipokuwa Trinidad siku baada ya kukabidhiwa zawadi ya dola 40,000 kwa kila kiongozi wa CFU.

"Wakati Mohamed Bin Hammam anataka kuja huku alikuwa anataka kuleta mapambo ya fedha, vikombe vya mbao na zawadi nyinginezo na kaniambia kuleta zawadi hizo kwa watu 30 itakuwa ni mzigo mkubwa. alisikika Warner katika video iliyotolewa.

"Nikamweleza hahitaji kuleta chochote lakini kama atahitaji kuleta chochote alete kitakacholingana na zawadi alizotaka kuleta. Nikawambia kama akija na fedha sitahitaji umpe mtu yoyote lakini kama ukitoa uwape viongozi wa CFU na wao ndio watazigawa kwa wajumbe. Kwasababu sitaki ieleweke kuwa unajaribu kuwanunua wajumbe hao ili wakupigie kura na alikubaliana nami." amesema wana katika sehemu ya taarifa  hiyo ya mkanda wa video.

 Warner pia alisema atarudisha fedha kama viongozi hawatazichukua.

EURO 2012 QUALIFIERS: SCOTLAND YAAGA RASMI MICHUANO HIYO.

NDOTO za timu ya Taifa ya Scotland kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwakani zilifutika baada ya kukubali kipigo kutoka kwa mabingwa watetezi Hispania cha mabao 3-1.

Magoli mawili yaliyofungwa na David Silva katika kipindi cha kwanza na bao la tatu la David Villa yalitosha kulizamisha jahazi la Scotland ambao walipata bao la kufutia machozi kutoka kwa David Goodwillie kwa penati dakika ya 66.

Scoland wamemaliza mchezo wao huo wa Kundi I wakiwa nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi 11 kwatika michezo nane waliyocheza.

Matokeo mengine ya michezo iliyochezwa jana ni kama ifuatavyo, Albania 1-1 Romania, Bulgaria 0-1 Wales, Croatia 2-0 Latvia, Denmark 2-1 Portugal, France 1-1 Bosnia-Hercegovina, Georgia 1-2 Greece, Germany 3-1 Belgium, Hungary 0-0 Finland, Italy 3-0 Northern Ireland, Kazakhstan 0-0 Austria, Lithuania 1-4 Czech Republic, Macedonia 1-1 Slovakia, Malta 0-2 Israel, Moldova 4-0 San Marino.

Mengine ni Norway 3-1 Cyprus, Rep of Ireland 2-1 Armenia, Russia 6-0 Andorra, Slovenia 1-0 Serbia, Sweden 3-2 Netherlands, Switzerland 2-0 Montenegro, Turkey 1-0 Azerbaijan.

Timu zilizokata tiketi ya kucheza michuano hiyo mpaka sasa ni pamoja na Poland, Ukraine, Germany, Russia,  Italy, France, Netherlands, Greece, England, Denmark, Spain, Sweden.

Wakati timu za Turkey, Republic of Ireland, Estonia, Bosnia-Hercegovina, Czech Republic, Croatia, Montenegro, Portugal zitalazimika kucheza hatua ya mtoano ili kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo, ratiba kwa ajili ya michezo ya mtoano itatolewa hapo kesho.

Tuesday, October 11, 2011

Quickest goal ever in the history of football (soccer) Mikhail Osinov

Morocco VS. Tanzania (3-1) Match summary

MISRI YAJITOA UENYEJI.

MISRI imejitoa kuandaa michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya Olympic.

Michuano hiyo yenye timu nane yalipangwa kuchezwa jijini Cairo kuanznia Novemba 26 mpaka Desemba 10 waka huu.

Timu tatu za juu ndizo zitakazoiwakilisha bara kwa ajili mashindano ya Olympic yatakayofanyika jijini London, Uingereza mwakani.

Misri tayari wamelifahamisha Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu uamuzi wake huo.

 Chama cha Soka cha nchi hiyo kimetoa uamuzi huo kutokana tatizo la usalama lilipo hivi sasa pamoja na uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Novemba.

Pamoja na Misri timu zingine zinazotarajiwa kushiriki katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Algeria, Gabon, Ivory Coast, Morocco, Nigeria, Senegal na Afrika Kusini.

VAN PERSIE KUULA ARSENAL.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal Robin van Persie huenda akaongezewa mkataba mrefu na na klabu yake hiyo ili kumbakisha mchezaji tegemeo.

Mchezaji huyo wa Kimataifa kutoka Uholanzi majaliwa yake ya kuwepo klabuni hapo yapo mashakani baada kukiri kuwa hahitaji kuongelea suala la mkataba mpya kwa hivi sasa mpaka msimu utapomalizika. Lakini Arsenal wako tayari kuvunja utaratibu wao wa malipo kwa wachezaji ili kuhakikisha wanampakisha nyota huyo.

Mkataba wa Van Persie unakwisha 2013 na Arsenal wanahitaji kumsainisha mkataba kabla ya msimu kumalizika. Klabu hiyo iliwapoteza nyota wake Samir Nasri na Gael Clichy mwaka huu baada kushindwa kufikia makubaliano hivyo hawataki hilo litokee kwa Van Persie.

Mchezaji huyo kwasasa analipwa paundi 70,000 kwa wiki lakini chanzo kimoja cha habari kutoka klabuni hapo kilitonya kuwa anaweza kuongezewa kiasi kikubwa zaidi ili kumbakisha. Nasri alikataa mshahara wa paundi 90,0000 kwa wiki na kujiunga na Manchester City na Arsenal wanaweza kumuongezea kiasi kama hicho mchezaji huyo.

Pia anaweza kupewa mkataba  wa miaka minne kitu ambapo kitakwenda kinyume na sera za klabu za kumpata mchezaji ambaye anakaribia miaka 30 mkataba mrefu kama huo.

Kwa miaka mingi Arsenal wamekuwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja kwa wachezaji walio na umri wa miaka 30 au zaidi, hata hivyo Kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger amevunja mwiko huo baada ya kumsainisha beki Sebastian Squillaci mkataba wa miaka mitatu ingawa ana miaka 30 na mchezaji kutoka Sevilla Mikel Arteta ambaye amepewa miaka mkataba wa miaka minne wakati anatimiza umri wa miaka 30 Machi mwakani.

Akiongea wiki iliyopita, Mtendaji Mkuu Ivan Gazidis alidokeza kuwa klabu hiyo ipo tayari kubadili utaratibu wake wa malipo ili kuwabakisha nyota wake.