![]() |
Raila Odinga, Waziri Mkuu wa Kenya. |
WAZIRI Mkuu wa Kenya amesema nchi hiyo inaweza kuandaa michuano ya kandanda ya Kombe la Dunia siku za karibuni.
Raila Odinga anataka nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 kabla haijajaribu kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia.
"Tutawekeza fedha zaidi siku zijazo katika kandanda nchini kwetu. Kusema kweli tunataka kujitokeza kuwania nafasi ya kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika," Odinga aliiambia BBC.
"Kenya ina uwezo na nafasi ya kuandaa si mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika lakini pia Kombe la Dunia."
Kenya ilikabiliwa na matatizo kadhaa ya kuandaa mashindano ya kimataifa kufuatia ajali ya mashabiki wa kandanda kukanyagana ambapo watu watano walikufa katika uwanja wa Nyayo mwaka jana.
Taarifa za awali zilisema mashabiki wanane walipoteza maisha yao lakini polisi wakatoa idadi nyingine ya watu waliokufa kuwa ni watano.
Bw Odinga amesema serikali ya Kenya itatengeneza miundo mbinu ya kandanda ili kutoa uhakikisho wa usalama kwa mashabiki hali itakayosaidia nchi hiyo kuweza kuandaa mashindano ya soka ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment