Thursday, May 2, 2013
DECO AKUTWA NA CHEMBECHEMBE ZA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.
KIUNGO wa klabu ya Fluminense ya Brazil, Deco ameshindwa kusafiri na timu yake hiyo kwenda Ecuador kwa ajili ya mechi ya Kombe la Libertadores baada ya kupimwa na kukutwa na chembechembe za dawa zilizopigwa marufuku michezoni. Katika taarifa iliyotumwa na katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa kwasasa hawawei kutoa taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo mpaka hapo watakapopata majibu ya vipimo vya mara ya pili ambavyo vinatarajiwa kutoka mapema kesho. Deco ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Porto, Barcelona na Chelsea amejitetea kwa kudai kuwa dawa za vitamin alizomeza ndizo zilizokuwa na vimelea vya dawa hizo. Amesema katika miaka 18 ya kucheza soka na miaka 15 kati ya hiyo akiwa barani Ulaya hajawahi kukutwa na tatizo kama hilo na huwa hana tabia ya kutumia dawa hizo.
No comments:
Post a Comment