Tuesday, September 17, 2013

NAHODHA WA ZAMANI GHANA AFARIKI DUNIA.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Emmanuel Quarshie amefariki dunia baada ya kuugua saratani ya koo kwa kipindi kirefu. Nahodha huyo alijulikana zaidi wakati alikiongoza kikosi cha Ghana maarufu kama Black Stars kushinda taji la Mataifa ya Afrika mwaka 1982. Miaka miwili baadae Quarshie aliendelea kung’ara zaidi wakati akicheza katika klabu ya Zamalek ya Misri kwa kuiwezesha klabu hiyo kunyakuwa taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Nguli huyo aliondoka Ghana Julai mwaka jana kwenda Misri kupatiwa matibabu ambapo klabu yake ya zamani ya Zamalek ilidhamini matibabu yake.

No comments:

Post a Comment