Tuesday, March 4, 2014

BARCELONA INAWEZA KUSHINDA MATAJI MATATU MSIMU HUU - FABREGAS.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas amedai kuwa hana shaka kwamba wanaweza kunyakuwa mataji matatu msimu huu. Barcelona kwasasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga wakiwa nyuma ya mahasimu wao Real Madrid kwa alama moja huku wakikaribia kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City na pia wakiwa wametinga fainali ya Kombe la Mfalme. Fabregas anakubali kuwa Barcelona bado haijafika katika kiwango chake cha juu lakini ana uhakika kuwa msimu huu unaweza kuwa na mafanikio kwao. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amesema bado wanatakiwa kukuza kiwnago chao cha uchezaji lakini kila kitu bado kiko ndani ya uwezo wao kwasababu bado wamebakiwa na mechi 19 mbele yao za ligi, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Mfalme na kama wakifanikiwa kushinda zote utakuwa msimu mzuri kwao.

No comments:

Post a Comment