MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Arsenal, Nicklas Bendtner amekiri kuwa hana furaha kwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Denmark ameanza mara moja pekee katika kikosi cha kwanza msimu huu na kocha Arsene Wenger hivi karibuni amekuwa akimchezesha Yaya Sanogo katika mechi muhimu za Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya kama akikosekana Olivier Giroud. Akizungumza katika kambi ya timu yake ya taifa kabla ya mchezo dhidi ya Uingereza utakaochezwa katika Uwanja wa Wembley kesho, Bendtner amesema yuko fiti kwa ajili ya kucheza na kama utamkuta mchezaji anapenda kusugua benchi anadhani ni bora atafute kazi nyingine. Bendtner amesema anataka kucheza na yuko tayari kwasababu anafanya mazoezi vizuri suala la kutochaguliwa na kocha sio juu yake.
No comments:
Post a Comment