Tuesday, March 4, 2014

MECHI YA BAFANA BAFANA DHIDI YA BRAZIL YAIVA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar jana ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo jijini Johannesburg akiongoza kundi la wachezaji wan chi hiyo wanaocheza soka Ulaya tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Bafana Bafana utakaochezwa kesho katika Uwanja wa FNB. Neymar alikuwa ameongozana na nyota wengine ambao ni Thiago Silva, Dante, Daniel Alves na Marcelo huku wengine wakiwemo viungo Fernandinho, Paulinho, Bernard na Hulk likiwa fungu la mwisho la wachezaji wanaocheza Ulaya kuwasili. Mashabiki walimiminika katika uwanja huo pamoja na hali ya manyunyu yaliyokuwa yakidondoka kwa ajili ya kumona nyota huyo wa Barcelona huku mmoja wao akifanikiwa kusogea karibu na kupiga picha naye kabla hajapanda katika basi lililokuwa likiwasubiri. Brazil ambayo inanolewa na kocha Luis Felipe Scolari inatarajiw akufanya mazoezi yao ya mwisho leo kabla ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment