MAOFISA kadhaa wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wamekamatwa kwenye msako wa polisi uliofanywa katika hoteli moja iliyopo jijini Zurich, Uswisi. Polisi walifika katika hoteli ya kifahari ya Baur au Lac mjini humo na wakaonekana wakiondoka na watu wawili. Katika taarifa yao FIFA wamesema mapema kuwa watashirikiana kikamilifu na wachunguzi na kuwa inafahamu hatua zilizochukuliwa leo na idara ya uchunguzi ya Marekani. Tarifa hiyo iliendelea kudai kuwa FIFA wataendelea kushirikiana kikamilifu na wachunguzi wa Marekani kama inavyokubalika katika sheria za Uswisi pamoja na uchunguzi unaoendeshwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa hoteli hiyo inayotumiwa na maofisa wa FIFA kuvamiwa na polisi mwaka huu huku tuhuma za ufisadi zikizidi kulizonga shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment