MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesisitiza kuwa anataka James Rodriguez abakie katika kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao. Rodriguez amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Madrid baada ya kuonekana kutokuwa katika mipango ya Zidane. Akihojiwa Zidane amesema kuna wachezaji wengi wanaocheza katika nafasi yake hivyo kunafanya uchaguzi wake kuwa mgumu. Hata hivyo, meneja huyo aliendelea kudai kuwa atakaa chini Rodriguez pindi atakaporejea kwani bado anamuhitaji katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment