Thursday, February 2, 2012
AFCON 2012: TIMU KUSIMAMA DAKIKA MOJA ZA MAOMBOLEZO.
TIMU zitasimama dakika moja kutoa heshima katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mashabiki walikufa na mamia kuumia katika vurugu za mashabiki zilizotokea nchini Misri Jumatano. Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF Issa Hayatou amesema kuwa soka la Afrika limekumbwa na janga kubwa na litakuwa katika maombolezo. Hayatou ambaye yupo nchini Guinea ya Ikweta katika jiji la Malabo kwa ajili ya mchezo wa Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Afrika kati ya Zambia na Sudan amesema CAF imetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Soka nchini humo-EFA kutokana na tukio hilo. Dakika moja za maombolezo zitafanyika katika michezo ya robo fainali zitakazochezwa katika miji ya Malabo, Bata, Libreville na Franceville. Watu wapatao 74 walikufa katika tukio hilo ambapo mashabiki walivamia uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini humo kati ya Al Masry na Al Ahly katika Uwanja wa Port Said.

No comments:
Post a Comment