Sunday, February 5, 2012
BAADA SERIKALI KUWAFUKUZA BODI NZIMA YA EFA YAAMUA KUJIUZULU.
RAIS wa Chama cha soka cha Misri-EFA Samir Zaher na bodi nzima ya Wakurugenzi wa chama hicho wamejiuzulu nyadhifa zao Jumamosi huku wakiwa tayari wamefukuzwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo kufuatia vurugu zilizosababisha zaidi ya watu 70 kupoteza maisha. Zaher pia ameripotiwa kuzuiwa kutoka nje ya Misri kutokana na uchunguzi unaoendelea kufuatia tukio baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka la nchi hiyo. Zaher na bodi yake walisema katika taarifa ya yao kwamba wamejiuzulu kwa pamoja kufuatia Waziri Mkuu Kamal el Ganzouri kuwafukuza kazi Alhamisi kufuatia tukio hilo kitendo ambacho serikali ingekuwa inaingilia mambo ya soka kitu ambacho Shirikisho la Soka Duniani-FIFA hawakiruhusu. Kujiuzulu huko walivyofanya viongozi hao Jumamosi ndio unaotarajiwa kupokewa na FIFA.

No comments:
Post a Comment