Wednesday, February 8, 2012
BREAKING NEWS: CAPELLO AJIUZULU.
KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amejiuzulu nafasi hiyo ya kukinoa kikosi hicho katika taarifa iliyotoka jana usiku. Hatua ya kocha huyo kujiuzulu imekuja kufuatia Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FA kumvua unahodha John Terry kutokana na kesi yake ya kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand. Capello aliachia wadhifa huo baada ya kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa FA David Bernastein na katibu wake Alex Horne huko Wembley. Katika taarifa iliyotolewa na FA imesema kwamba mazungumzo yalikuwa ni juu ya suala ya Terry kuvuliwa unahodha pamoja na kauli aliyotoa Capello wakati akihojiwa na vyombo vya habari nchini Italia kuhusiana na suala hilo. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa baada ya mazungumzo yaliyochukua zaidi ya muda wa saa moja hatimae FA ilikubali ombi la kujiuzulu la kocha huyo ambaye ameachia nafasi hiyo na kumshukuru katika kipindi chote alipokuwa akikinoa kikosi hicho. Kwasasa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana chini ya miaka 21 Stuart Pearce ndio atachukua mikoba ya kukiongoza kikosi hicho katika mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Uholanzi Februari 29 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment