Friday, February 10, 2012
CHU-YOUNG AITWA KIKOSI CHA KOREA KUSINI.
MCHEZAJI wa Arsenal Park Chu-Young ni mmoja kati ya wachezaji watatu ambao hawachezi ligi ya nyumbani kwao kuitwa na kocha Choi Kang-Hee katika timu ya taifa ya Korea Kusini kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uzbekistan ili kujiwinda na mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Kuwait. Korea Kusini imefungana kwa alama na Lebanon katika kundi B wote wakiwa na alama 10 lakini wakiongoza kwa tofauti ya mabao watahitaji hata sare katika mchezo wao dhidi ya Kuwait ili kujihakikishia nafasi ya juu katika mzunguko wa mwisho wa kundi hilo ambao utaanza June mwaka huu. Choi ambaye mwaka uliopita alikuwa akikinoa kikosi cha Jeonbuk Motors ambacho kilinyakuwa ubingwa wa ligi kuu ya nchini humo maarufu kama K-League na kushika nafasi ya pili katika michuano ya Klabu Bingwa ya bara la Asia alichukua mikoba ya kukinoa kikosi cha nchi hiyo baada ya kocha Cho Kwang-Rae kutimuliwa kutokana na matokeo mabaya. Mbali na Park wengine walioitwa ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi yao ni pamoja na Lee Jung-Soo anayekipiga timu ya Al Sadd ya Falme za Kiarabu na Ki Sung-Yueng anayecheza Celtic ya Scotland wakati wachezaji wengine wtano walioitwa wanatoka timu ya Jeonbuk Motors ambayo Choi alikuwa akifundisha.

No comments:
Post a Comment