Friday, February 3, 2012
FA KUJADILI JUU YA KUMVUA UNAHODHA TERRY.
SHIRIKISHO la Soka la Uingereza-FA wako katika majadiliano juu nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo John Terry kama aendelee kuingoza timu hiyo au wamvue wadhifa huo wakati akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake ambapo anatuhumiwa kwa kutoa kauli za kibaguzi. Terry ambaye kesi yake ilisikilizwa Jumatano alikatana kutenda kosa hilo la kumtolea maneno ya kibaguzi beki wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand wakati wa mchezo wa Ligi Kuu wan chi hiyo. Terry ambaye pia ni nahodha wa Chelsea kesi yake itasikilizwa tena Julai mwaka huu baada ya michuano ya Kombe la Ulaya ambapo mchezaji anatarjiwa kuwepo katika kikosi hicho pamoja na kaka wa Anton anayechezea klabu Manchester United Rio Ferdinand. Kocha wa timu ya taifa a nchi hiyo Fabio Capello amekuwa akimkingia kifua nahodha wake huyo akidai kwamba hana hatia mpaka hapo itakapothibitika kwamba ni kweli alifanya kosa hilo.

No comments:
Post a Comment