Friday, February 3, 2012
KOCHA AL AHLY ATAKA KUACHIA NGAZI.
BAADA ya kupigwa na wahuni juzi kocha wa klabu ya Al Ahly Manuel Jose ameomba kuvunja mkataba wake ambapo amesema anajiandaa kuondoka nchini kwao Ureno huku akifikiria suala la kustaafu kazi hiyo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo kocha huyo amesema kuwa maisha ni mafupi na kwa jinsi alivyoshuhudia mashabiki wakiuwawa mbele yake anahitaji kuangalia upya suala la maisha yake. Kwasasa nchi nzima ya Misri na mashabiki wa mpira duniani kote bado wako katika mshtuko kuhusiana na tukio hilo ambalo lilichukua maisha ya watu wapatao 74. Wakihojiwa kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Al Ahly Abd El Hafez amesema kuwa siku ya tukio hilo ni baya kuwahi kumtokea katika maisha yake wakati mshambuliaji nyota wa Zamalek ameonya kuwa hawezi kucheza mpira kama vitendo kama hivyo hivyo vitaendelea kufumbiwa macho. Naye mchezaji wa El Masry ambao mashabiki wao ndio wanatuhumiwa kuanzisha vurumai hizo Mahmoud Abdel Hakim akihojiwa huku machozi yakimtoka amesema anaona haya kwa tukio hilo na hatamani kumtizama mtu yoyote usoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment