Sunday, February 5, 2012
MMILIKI WA NOTTIGHAM FOREST AKUTWA AMEKUFA.
MMILIKI wa klabu ya Nottingham Forest Nigel Doughty amekutwa amekufa katika chumba cha kufanyia mazoezi nyumbani kwake Skillington, Lincolnshire nchini Uingereza. Mwezi Octoba mwaka jana Doughty ambaye alikuwa na miaka 54 alitangaza kuwa angejiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti wa klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu. Bosi huyo wa Nottingham aliinunua klabu hiyo mwaka 1999 kwa paundi milioni 11 ambapo aliokoa timu hiyo iliyokuwa ikikaribia kufilisika na kuchukua madaraka ya uenyekiti rasmi miaka mitatu baadae kutoka kwa Eric Barnes. Katika miaka 10 akiwa mmiliki wa klabu hiyo ameiwezesha kushinda michuano ya Ligi Daraja la kwanza mwaka 2008 wakiwa chini ya kocha Billy Davies ambaye baadae alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Steve McClaren. McClaren hakukaa sana na klabu hiyo baada ya kujiuzulu Octoba mwaka jana kwa madai mshahara mdogo aliokuwa akipewa.

No comments:
Post a Comment