OZIL ATAKA KUMALIZIA SOKA LAKE BERNABEU.
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Mesut Ozil amesema kuwa ana matumaini ya kubakia katika klabu hiyo katika kipindi chote cha uchezaji wake soka. Ozil mwenye umri wa miaka 23 alitua Bernabeu akitokea klabu ya Werder Bremen baada kuingoza Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ambapo amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Mourinho. Akihojiwa mchezaji huyo amesema kuwa anahitaji kumalizia kucheza soka akiwa na klabu hiyo ingawa anajua bado miaka mingi mbele na itakuwa vigumu kwasababu watakuja wachezaji wengi katika miaka ijayo ambao watakuwa wazuri. Ozil pia anaamini kuwa msimu huu utaisha timu yake wakiwa mabingwa kama wataendelea kucheza kama wanavyocheza hivi sasa hakuna anayeweza kuwapita.
No comments:
Post a Comment