Thursday, February 9, 2012

REDKNAPP ATAJWA KUVAA VIATU VYA CAPELLO.

KUJIUZULU kwa kocha wa Uingereza Fabio Capello imekuwa ni habari ambayo imetikisa soka la nchi hiyo huku kocha wa Tottenham Hotspurs Harry Redknapp akipewa nafasi kubwa ya kuvaa viatu vya Capello. Kuondoka kwa Capello kufuatia sakata la beki wa timu hiyo John Terry kuvuliwa unahodha inamaanisha Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FA inabidi liteue kocha mwingine haraka kufuatia miezi minne tu iliyobakia kabla ya michuano ya Kombe la Ulaya itakayofanyika Poland na Ukraine mwezi June mwaka huu. FA italazimika kuziba nafasi hiyo kabla ya mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uholanzi utakaofanyika Wembley Februari 29 mwaka huu. Stuart Pearce ambaye ni kocha wa sasa wa kikosi cha Uingereza cha vijana chini ya miaka 21 na alikuwa msaidizi wa Capello katika kikosi cha wakubwa ndiye atakinoa kikosi katika kipindi kifupi hiki lakini jina Redknapp ndio linatajwa kama kocha atakaekinoa kikosi hicho kwa kipindi kirefu kijacho.

No comments:

Post a Comment