Tuesday, February 7, 2012
SIR BOBBY CHARLTON AFANYIWA UPASUAJI MDOGO.
MCHEZAJI nguli wa zamani wa Manchester Bobby Charlton amefanyiwa upasuaji mdogo Jumatatu ambao ulimzuia kupokea tuzo ya heshima kutambua mchango wake katika soka iitwayo Laureus Sports awards. Charlton mwenye umri wa miaka 74 ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na timu ya Uingereza mwaka 1966 na miaka miwili baadae kushinda Kombe la Ulaya akiwa na Manchester United aliumwa Jumapili na kurejea jijini Manchester. Kocha wa Mnchester United Sir Alex Ferguson alipokea tuzo hiyo kwa niaba yake ikiwa ni miaka 54 imepita baada ya Charlton kupona katika ajali ndege iliyotokea jijini Munich ambapo wachezaji nane wa timu ya Manchester United walifariki. Charlton alijiunga na klabu ya Manchester toka akiwa na umri wa miaka 15 na toka kipindi hiko amekuwa sehemu ya klabu na pia alikuwa sehemu ya watu waliomteua Ferguson kuinoa klabu hiyo mwaka 1986.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment