Thursday, February 2, 2012
WAFANYAKAZI WAGOMA NCHINI BRAZIL.
WAFANYAKAZI wanaofanya kazi katika viwanja vitakavyotumia katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil wamegoma wakidai kuongezwa mshahara katika mji wa Salvador uliopo Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA Jerome Valcke aliusifia mji huo kwa maandalizi mazuri wiki mbili zilizopita alipofanya ziara nchini humo lakini wafanyakazi walikuwa hawana furaha kutokana na mikataba iliwekwa kati ya miji itayaoandaa michuano hiyo na kampuni zilizopewa tenda ya kujenga viwanja hivyo. Uwanja wa Arena Fonte Nova uliopo jijini Salvador pia ni moja ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Confederations Cup michuano ambayo hufanyika mwaka mmoja kabla ya michuano ya Kombe la Dunia ambapo utahitajika uwe tayari katika muda mzuri ili uweze kutumika kwa mashindano hayo June 2013. Brasilia, Belo Horizonte na Rio de Janeiro miji yote hiyo nayo ilikubwa na tatizo kama hilo la migomo kwa wafanyakazi mapema katika maandalizi yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment