Sunday, February 5, 2012
WENGER KUMUONGEZA MKATABA HENRY.
MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger huenda akajaribu kuongeza mkataba wa Thierry Henry aliyetua klabuni hapo kwa mkopo akitokea New York Red Bulls. Katika mkataba wake Henry amebakisha wiki moja ambapo mchezo wake wa mwisho unatarajiwa kuwa dhidi ya Sunderland Jumamosi ijayo pamoja na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Februari 15 dhidi ya AC Milan kabla ya kurejea Marekani. Wenger amesema timu yake bado haijafanya mazungumzo yoyote juu ya kuongeza mkataba na Red Bulls lakini akafafanua kuwa inawezekana wakafanya hivyo. Kocha huyo alindelea kusema kuwa kama wakiamua kuongeza mkataba itakuwa na kwa wiki zingine mbili hivyo kumfanya mshambuliaji huyo kuwemo katika kikosi hicho kitakachocheza dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Tottenham Hotspurs katika Kombe la FA Februari 26.

No comments:
Post a Comment