Wednesday, July 18, 2012

NIKO FITI KWA AJILI YA OLIMPIKI - BLAKE.

Yohane Blake.
MWANARIDHA nyota Yohane Blake amesema kuwa kwasasa yuko tayari kwa ajili ya michuano ya Olimpiki baada ya kushinda mbio za mita 100 zilizofanyika jijini Lucerne, Switzerland akitumia muda wa sekunde 9.85. Blake ambaye ana miaka 22 ambaye ndiye anashikilia rekodi ya mkimbiaji mwenye kasi zaidi kwa mwaka huu, ameonyesha kuwa kwanini anatabiriwa kuwa tishio kwa bingwa mtetezi wa mbio za mita 100 na 200 kwenye michuano ya olimpiki, Usain Bolt. Ni Bolt mwenye sekunde 9.76 na bingwa wa olimpiki mwaka 2004 Justin Gatlin sekunde 9.80 pekee ndio wanariadha waliokimbia haraka zaidi kwa mwaka huu. Blake alimshangaza Bolt katika fainali ya mbio za mita 100 za mchujo wa olimpiki nchini Jamaica zilizofanyika mwezi uliopita ambapo alishinda mbio hizo kwa kutumia sekunde 9.75 ukiwa ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Mwanariadha huyo hakuishia hapo bali pia alimshinda Bolt katika mbio za mita 200 akitumia muda wa sekunde 19.80.

No comments:

Post a Comment