TUHUMA MPYA ZA RUSHWA ZAMWANDAMA BIN HAMMAM.
 |
| Mohammed bin Hammam. |
CHAMA cha Soka barani Asia-AFC kinamtuhumu rais wa chama hicho Mohammed bin Hammam kwa rushwa baada ya kufanyika mahesabu ya ndani na kugundua kuna baadhi ya hela hazieleweki zilipopelekwa. Katika taarifa yake AFC wamesema kuwa wamelazimika kumsimamisha kwa siku 30 Bin Hammam ambaye tayari anapambana na kifungo cha maisha kujishughulisha na masuala ya soka alichopewa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA. Tuhuma hizo mpya zinaongeza aibu kwa Bin Hammam raia wa Qatar ambaye aliondolewa katika kinyang’anyiro cha urais wa FIFA baada ya kujaribu kununua kura wakati akipambana na rais wa shirikisho hilo mwaka uliopita. Taarifa ya chama hicho chenye makao yake makuu nchini Malaysia zimesema kuwa vikwazo vya hivi karibuni dhidi ya Bin Hammam vimekuja baada ya ukaguzi wa mwaka mzima uliofanywa na kubaini ukandamizaji kuhusu utekelezaji wa baadhi ya mikataba na kuifanya akaunti ya benki ya AFC kama mali yake. Taarifa hiyo haikutoa hakufafanunua vizuri zaidi ya kusema kuwa suala hilo limepelekwa katika kamati ya maadili ya AFC. Bin Hammam alichaguliwa rais wa AFC mwaka 2002 na kwa hivi sasa amekuwa akipambana kusafisha jina lake toka alipokumbwa na kashfa ya rushwa Mei mwaka 2011 ikiwa ni wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais wa FIFA.
No comments:
Post a Comment