Wednesday, June 4, 2014

BECKHAM ADOKEZA KUREJEA UWANJANI.

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, David Beckham amedokeza kuwa anaweza kujiandaa kurejea tena uwanjani baada ya kustaafu. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 hajacheza soka la ushindani toka alipotundika daruga zake Mei mwaka jana akiwa katika klabu ya Paris Saint-Germain. Toka wakati huo ametangaza mpango wake wa kuzindua klabu yake itakayokuwa ikishiriki Ligi Kuu nchini Marekani-MLS ambayo itakuwa na maskani yake jijini Miami. Beckham ameiambia BBC kuwa hivi sasa amekuwa akienda kutizama mechi za mpira wa kikapu na wakati akitizama wachezaji amekuwa akivutiwa kurejea tena uwanjani kucheza. Hata hivyo pamoja na kupitiwa na wazo la kurejea uwanjani lakini amekuwa akijiuliza kama ataweza kucheza tena baada ya kustaafu. MLS imekuwa ikivutia nyota mbalimbali katikammiaka ya karibuni huku Beckham mwenye akiwa amewahi kuichezea timu ya Los Angeles Galaxy sambamba na nyota wengine kama Robbie Keane na Thierry Henry wote wakiwa wamecheza ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment