Monday, June 9, 2014

CAMEROON WAKUBALI KWENDA BRAZIL BAADA YA KUTATULIWA MGOGORO WA POSHO.

HATIMAYE kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon wamesafiri jana kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutatuliwa mgogoro wa posho zao. Kikosi hicho akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Samuel Eto’o waligoma kusafiri kuelekea katika michuano hiyo jana asubuhi. Lakini baadae walikubaliana kuhusu malipo na Shirikisho la Soka la nchi hiyo baada ya kufanyika kwa mkutano wa dharura. Baada ya makubaliano hayo kikosi hicho kilipanda ndege usiku kikiwa kimechelewa kwa saa 12 kutokana na mgogoro huo. Kocha wa timu hiyo Volker Finke amesema wachezaji wake walikuwa wamedai kiasi cha paundi 61,000 walichotakiwa kupewa kulikuwa kidogo sana kwa ajili ya michuano hiyo. Cameroon imepangwa kundi A sambamba na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.

No comments:

Post a Comment