KIONGOZI wa kiroho wa Kanisa Katoliki, Papa Francis anatumaini michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kutimua vumbi baadae leo, itachezwa kwa imani, udugu na haki huku akitaka iwe kilelezo cha mshikamano miongoni mwa watu. Katika ujumbe wake uliotolewa kwenye video kwa lugha ya Kireno kuwaendelea mashabiki na waandaji wa michuano hiyo nchini Brazil, Papa Francis ambaye ni raia wa Argentina amesema michezo haijawekwa kwa ajili ya kufurahisha pekee bali pia kukuza mema na kujenga undugu na amani katika jamii. Papa amesema ni matumaini yake kuwa mbali na michuano hiyo kuwa sikukuu ya michezo, Kombe la Dunia linaweza kuwa sikukuu ya mshikamano miongoni mwa watu. Papa aliongeza kuwa michezo ni shule ya amani na inawafundisha kujenga amani.

No comments:
Post a Comment