Monday, June 9, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: VURUGU ZAIDI ZA MAANDAMANO ZARINDIMA BRAZIL.

POLICE nchini Brazil wamelazimika kutumia mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji katika jiji la Sao Paulo ikiwa ni siku tatu kabla ya michuano ya Kombe la Dunia haijaanza kutimua vumbi mchezo wa ufunguzi katika mji huo. Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Katy Watson aliyekuwepo eneo la tukio amedai kuwa zaidi ya waandamanaji 300 alikuwepo mtaani na helikopta zilikuwa zikizunguka juu yao. Waandamanaji hao waliitwa na wafanyakazi wa Sao Paulo ambao waligoma kuunga mkono ongezeko la asilimia 12.2 la mshahara. Rais wa Brazil Dilma Rousseff amesema hataruhusu vurugu ya vurugu kuingilia michuano ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment