Wednesday, June 11, 2014

LAHM, MULLER WAONGEZA MKATABA BAYERN.

WACHEZAJI nyota Philipp Lahm na Thomas Muller wamesaini mkataba mpya wa miaka miwili kila mmoja na klabu ya Bayern Munich. Nahodha Lahm sasa ataendelea kubakia kwa mabingwa hao wa Bundesliga mpaka Juni mwaka 2018 wakati Muller ambaye alihisiwa kuondoka naye ataendelea kubakia hapo mpaka Juni mwaka 2019. Wachezaji wote wawili walitoka katika timu ya vijana ya Bayern na Ofisa Mkuu wa timu hiyo Karl-Heinz Rummenigge alipongeza uamuzi wa wachezaji hao kubakia. Rummenigge aliuambia mtandao wa timu hiyo kuwa wachezaji hao wamekuwa sehemu muhimu katika ustawi wa maendeleo wa klabu hiyo na kukubalia kwao kuongeza mkataba ni kuonyesha jinsi gani walivyokuwa waaminifu. Lahm mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Bayern akiwa na umri wa miaka 11 na amefurahishwa kwa kupewa nafasi ya kumalizia soka lake akiwa hapo Allianz Arena.

No comments:

Post a Comment