Tuesday, June 3, 2014

LAMPARD AAMUA KUACHANA NA CHELSEA.

KIUNGO mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard ametangaza kuondoka katika timu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 13. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 35, mfungaji bora wa klabu hiyo akiwa na mabao 211 mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi huu. Toka ajiunge nao akitokea West Ham United mwaka 2001, Lampard ameshinda mataji 11 yakiwemo mataji matatu ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya waliloshinda mwaka 2012. Lampard ambaye anaweza kuamua kutundika daruga lakini amepata ofa kutoka vilabu 16 tofauti amesema Chelsea imekuwa sehemu ya maisha yake. Pamoaj na kuthibitisha kwamba ataondoka Chelsea, Lampard ambaye yupo katika kikosi cha timu ya taifa amesema hawezi kusema chochote kuhusu mstakabali wake kutokea hapo mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment