KLABU ya Liverpool imewasilisha mpango wake wa kuendeleza Uwanja wa Anfield na kuupanua ili uwe na uwezo wa kuingiza mashabiki 58,000. Klabu hiyo ilibainisha kuwa mpango wake huo wameuwasilisha katika manispaa ya mji huko jana. Kama wakipewa kibali klabu hiyo wa Ligi Kuu itaongeza idadi ya viti katika majukwaa yote kubwa na lile la Anfield Road ambapo wamepanga kuukamilisha katika msimu wa 2016-2017. Kwa upande wa jukwaa kuu wamepanga kuongeza siti 8,500 hivyo kuongeza uwezo wa kuchukua mashabiki kupifikia 21,000 huku lile jukwaa la Anfield Road likitarajiwa kuongezwa siti 4,800 hivyo kutimiza jumla ya mashabiki 58,800. Mpango wote huo wa kuongeza baadhi ya maeneo unakadiriwa kufikia kiasi cha paundi milioni 260 huku ukitoa fursa ya ajira zaidi ya 100.

No comments:
Post a Comment