Tuesday, June 3, 2014

MAN CITY YAMTENGEA FABREGAS EURO MILIONI 37.

KLABU ya Manchester City inajiandaa kutenga kitita cha euro milioni 37 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas. Mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Uingereza wameamua kutoa kitita hicho rasmi kwa kiungo huyo ambaye ameambiwa anaweza kuondoka Camp Nou majira haya ya kiangazi. Wakati City wakionekana wako tayari kuipata saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 klabu yake ya zamani Arsenal nao wanaonekana bado wanamfuatilia kwa ajili ya kumrejesha tena Emirates. Mbali na timu hizo, Liverpool na Chelsea nao pia wameonyesha kufuatilia nyendo za nyota huyo hukususani kwa Chelsea ambapo Frank Lampard amethibitisha kuondoka. City wanamuwinda kiungo huyo kutokana na kutokuwa na uhakika wa kuwa na Yaya Toure kwa msimu ujao baada ya kiungo huyo kudai hana furaha Etihad.

No comments:

Post a Comment