Tuesday, June 3, 2014

ROAD TI BRAZIL: NIGERIA YATANGAZA SILAHA ZAKE.

KIUNGO Nosa Igiebor ni miongoni mwa wachezaji saba waliopigwa chini katika kikosi cha wachezaji 23 wa mwisho wa Nigeria kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia. Nyota wa Real Betis na kiungo wa Parma Joel Obi ambao wote walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Scotland na kutoka sare ya mabao 2-2 wote wamekuwa wakiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara msimu huu. Winga wa zamani wa West Ham United, Victor Obinna naye ameenguliwa kutokana na matatizo ya majeraha. Nyota wa klabu ya Bastia Sunday Mba pia ameachwa katika kikosi hicho pamoja na kufunga bao la ushindi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana. Wengine waliokosekana katika kikosi hicho ni pamoja na golikipa Daniel Akpeyi, na viungo Ejike Uzoenyi na Nnamdi Oduamadi. Mabingwa hao mara tatu wa Afrika wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ugiriki baadae leo huko Philadelphia, na baadae Juni 7 watacheza na Marekani huko Jacksonville, Florida kabla ya kusafiri kuelekea jijini Sao Paulo. Nigeria inakabiliwa na kibarua kigumu katika kundi F ambapo itachuana na timu za Argentina, Iran na Bosnia.

Kikosi Kamili ni
Makipa: Vincent Enyeama (Lille), Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheva), Chigozie Agbim (Gombe United).
Mabeki: Elderson Echiejile (Monaco), Efe Ambrose (Celtic), Godfrey Oboabona (Rizespor), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), Kenneth Omeruo (Middlesbrough), Juwon Oshaniwa (Ashdod), Joseph Yobo (Norwich, on loan from Fenerbahce), Kunle Odunlami (Sunshine Stars).
Viungo: John Mikel Obi (Chelsea), Ramon Azeez (Almeria), Ogenyi Onazi (Lazio), Reuben Gabriel (Waasland-Beveren), Michael Babatunde (Volyn Lutsk).
Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow), Shola Ameobi (Newcastle), Emmanuel Emenike (Fenerbahce), Michael Uchebo (Cercle Brugge), Peter Odemwingie (Stoke), Victor Moses (Liverpool, on loan from Chelsea), Uche Nwofor (Heerenveen).


No comments:

Post a Comment