Wednesday, June 11, 2014

RONALDO AWAPOZA MASHABIKI WA URENO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amewahakikishia mashabiki wa soka wan chi kuwa anatarajia kuwa fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya kucheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Jamhuri ya Ireland ambao walishinda kwa mabao 5-1.  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akiandamwa na majeruhi ya hapa na pale toka klabu yake ya Real Madrid ishinde mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico, na kulikuwa na hofu kuwa anaweza kuungana na Marco Reus, Franck Ribery na Radamel Falcao kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokosa michuano hiyo. Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alipangwa katika kikosi cha kwanza cha Ureno kinachonolewa na Paulo Bento katika mchezo huo uliofanyika huko New Jersey, Marekani jana usiku na kucheza kwa dakika 65 kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Nani. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ronaldo amesema kwasasa ameanza mazoezi vyema huku akifuatilia ushauri aliopewa na madaktari hivyo ni mategemeo yake mpaka muda wa mashindano atakuwa fiti kwa asilimia 100. Ureno inakabiliwia na kibarua kigumu kwa kundi G lililokuwa na timu kama Ujerumani, Marekani na Ghana.

No comments:

Post a Comment