Wednesday, June 11, 2014

SAN ANTONIO SPURS YAZIDI KUIKALIA KOONI MIAMI HEAT KATIKA FAINALI ZA NBA.

TIMU ya mpira wa kikapu ya San Antonio Spurs imerejea kwenye usukani wa kuongoza kwa 2-1 baada ya kufanikiwa kuifunga Miami Heat kwa vikapu 111-92 katika fainali ya tatu kati saba watakazocheza ya ligi ya mchezo huo-NBA. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Heat kupoteza mechi ya nyumbani katika hatua za mtoano mchezo ambao mchezaji nyota mwenye thamani zaidi wa NBA LeBron James na Dwyane Wade wote walifunga vikapu 22 kila mmoja. Kwa upande wa Spurs, Kawhi Leonard ndiye aliyefunga vikapu vingi zaidi 29 katika mchezo huo ambao walionyesha kuumiliki toka mwanzoni. Fainali ya nne ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho.

No comments:

Post a Comment