SERIKALI ya kijeshi ya Thailand imeamuru luninga zote nchini humo kuhakikisha mashabiki wa soka hawalipii kutizama mechi yoyote ya Kombe la Dunia. Uongozi huo wa kijeshi umedai hiyo ni hatua ya kampeni zake za furaha ambazo zimeshuhudia mambo mbalimbali ikiwemo watu kunyolewa nywele bure na matamasha ya bure. Kwa upande mwingine kiongozi wa waandamanaji wanaopinga uongozi wa kijeshi ameshitakiwa kwa kosa la uchochezi na atakabiliwa na kifungo cha miaka 14 jela kama akikutwa na hatia. Jeshi la nchi hiyo lilitwaa madaraka kutoka kwa serikali ya kiraia mwezi uliopita na kuahidi kuweka mambo sawa kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine wa kiraia huku mji kama Bangkok na sehemu nyingine za nchi hiyo kukiwa na amri ya kutotoka nje.

No comments:
Post a Comment