DORTMUND YAMNASA GINTER.
KLABU ya Borussia Dortmund imefanikiwa kukamilisha usajili wa Matthias Ginter kutoka Freiburg kwa uhamisho unaoaminika kufikia euro milioni 10. Rais wa Freiburg, Freiz Keller alibainisha mapema wiki hii kuwa mazungumzo yalikuwa yamefikia mahali pazuri na sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 amesaini mkataba utakaomalizika Juni mwaka 2019 baada ya kufaulu vipimo vya afya. Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc amesema wamekuwa wakimuwinda kinda huyo wa kimataifa wa Ujerumani kwa kipindi kirefu hivyo amefurahi kuwa hatimaye amechagua kujiunga nao. Ginter ambaye alikuwemo katika kikosi cha Ujerumani kilichotawadhwa mabingwa wa dunia mwishoni mwa wiki iliyopita alitokea katika shule ya Freiburg na alianza kutokeza katika kikosi cha kwanza mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment