Wednesday, July 9, 2014

ETO'O AMVALISHA PETE MCHUMBA WAKE WA SIKU NYINGI.

MSHAMBUALIAJI nyota na nahodha wa timu ya Ivory Coast, Samuel Eto’o ameamua kumchumbia mpenzi wake wa siku nyingi na mama wa watoto wake wawili Tra Lou Georgette kwa ajili ya kufunga nae ndoa. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea, Georgette na watoto wao wawili waliwasili jijini Abidjan mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya sherehe fupi ya kuvishana pete ya uchumba wakati ambao Eto’o alimvalisha mke wake huyo mtarajiwa pete ya almasi yenye thamani ya euro 500,000. Hakuna tarehe yoyote rasmi iliyotajw akwa ajili ya harusi lakini ndugu wa familia ya Geogette wamesema itatangazwa rasmi katika kipindi kifupi kijacho. Wawili hao ambao wamekuwa katika mahusiano kwa kipindi cha miaka tisa, wamewahi kufunga ndoa ya kimila mwaka 2007 lakini walikuwa bado hawajafunga ndoa ya kanisani. Hii siyo mara ya kwanza kwa Eto’o kumpa vito vya thamani mpenzi wake huyo, kwani mwaka 2008 alimnunulia kidani cha shingoni katika siku yake ya kuzaliwa ambacho kilikuwa na thamani ya euro 152,500.

No comments:

Post a Comment