Thursday, July 17, 2014

FABREGAS ANAWEZA KUVAA VIATU VYA LAMPARD - TERRY.

BEKI mahiri wa klabu ya Chelsea, John Terry ana uhakika kuwa Cesc Fabregas anaweza kuchukua nafasi ya Frank Lampard katika timu hiyo msimu huu. Fabregas amesajiliwa kutoka Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano uliowagharimu kiasi cha euro milioni 38 na Terry ana uhakika kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania anaweza kuvaa viatu vya Lampard. Terry amesema usajili wa Fabregas ni mzuri na anamkumbuka wakati akiwa Arsenal kwani alikuwa ana uwezo mkubwa anapokuwa na mpira na pia ni mfungaji mzuri. Lampard alitangaza uamuzi wake wa kuondoka Chelsea, Juni mwaka huu na terry amakiri alishtushwa kuona mmoja wa marafiki wake wa karibu pamoja na Ashley Cole wakiondoka Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment