WINGA mahiri wa klabu ya Argentina Angel Di Maria ameanza mazoezi jana kwa mategemeo ya kuwepo katika mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani pamoja na kupata majeruhi ya msuli siku chache zilizopita. Di Maria mmoja wachezaji wazuri kabisa katika bara la Amerika Kusini baada ya Lionel Messi, aliumia msuli wakati akipiga shuti wakati wa mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Ubelgiji. Winga huyo mwenye kasi anayekipiga katika klabu ta Real Madrid, ambaye huwa anaelewana vyema na Messi katika safu ya ushambuliaji ya Argentina alianza mazoezi mepesi jana kwa mara ya kwanza toka aumie. Hata hivyo hofu sio kubwa sana hata kama Di Maria hatakuwa fiti kwa asilimia 100 kutokana na mshambuliaji Sergio Aguero naye kupona kabisa kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Argentina inatarajiw akusafiri kuelekea jijini Rio de Janeiro kesho kwa ajili ya mchezo huo.

No comments:
Post a Comment