Thursday, July 10, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: MESSI ATOA USHINDI WA JANA KWA MWANDISHI WA ARGENTINA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI HUKO BRAZIL.

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ametoa ushindi wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia waliopata dhidi ya Uholanzi jana kwa mwandishi wa habari wan chi hiyo ambaye alikufa katika ajali ya barabarani asubuhi siku ya mchezo. Mwandishi huyo Jorge Lopez ambaye alikuwa akiripoti michuano hiyo kupitia redio ya La Red, alikufa wakati gari lililoibiwa lilipokuwa likifukuzana na polisi kabla ya kuigonga taxi aliyokuwa amepanda wakati akielekea hotelini kwake. Mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 38 amewahi kufanya kazi jijini Barcelona katika gazeti la moja la michezo, ambapo alikuwa mwandishi anayehusudiwa na Messi. Messi alituma salamu zake za rambirambi kwa mwandishi huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, na kudai ushindi huo ni maalumu kwa ajili yake huku akitoa pole kwa familia yake kwa kuondokewa na mpendwa wao. Argentina sasa itakwaana na Ujerumani katika mchezowa fainali utakaochezwa Jumapili hii katika Uwanja wa Maracana uliopo katika jiji la Rio de Janeiro.

No comments:

Post a Comment