Friday, July 11, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: PAMOJA NA KUIPIKU REKODI YAKE KLOSE AMVULIA KOFIA RONALDO.

MSHAMBULIAJI mkongwe wa timu ya taifa ya Ujerumani, Miroslav Klose, amempongeza Ronaldo baada ya kuipiku rekodi ya mabao ya nyota huyo wa zamani wa Brazil na kuisaidia nchi yake kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 alifunga bao lake la 16 katika michuano ya Kombe la Dunia kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil huko Belo Horizonte Jumanne iliyopita ambapo Ujerumani iliwagaragaza weyeji hao mabao 7-1. Akihojiwa na waandishi wa habari katika kambi yao ya mazoezi, Klose amesema pamoja na kumzidi nguli huyo kwa mabao lakini anamtambua kama mmoja wa wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika soka. Klose aliendelea kudai kwasasa anacheza soka nchini Italia na kila mtu huko anasema Ronaldo ni mchezaji bora kabisa kuwahi kucheza soka nchini humo. Ujerumani sasa watakwaana na Argentina katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia utakaofanyika katika Uwanja wa Maracana Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment