KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amesema hakuna uamuzi wowote atakaofanya kuhusu nafasi yake katika timu hiyo mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia. Pamoja na kipigo cha fedheha cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali Jumanne iliyopita, Scolari amesema atafikiria kuhusu mustakabali wake mara baada ya mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Uholanzi Jumamosi hii. Scolari amesema bado wana kazi ya kufanya kwasababu bado wana majukumu waliyopewa na Shirikisho la Soka la Brazil mpaka michuano hiyo itakapomalizika. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mpaka kufikia Jumamosi baada ya mchezo huo ndio anaweza kuzungumzia hatma yake.

No comments:
Post a Comment